Tunaunda Odoo kulingana na jinsi maeneo yako ya ujenzi yanavyofanya kazi tayari — misimbo yako ya gharama, wasambazaji wako, taratibu zako za kuidhinisha — kisha tunaifundisha timu yako hadi iweze kuendesha mfumo bila sisi.
Kila mradi kwenye skrini moja
Miradi, kazi na timu za eneo la ujenzi pamoja. Gawa kila mradi katika hatua kama msingi, muundo na umaliziaji, panga timu za kazi, na ufuatilie maendeleo, manunuzi na matumizi ya eneo hilo kwenye ukurasa mmoja wa mradi.

Jua kilichopo kwenye eneo la kazi
Manunuzi yanayounganishwa na mradi. Omba bei kutoka kwa wasambazaji kulingana na mahitaji ya kila eneo la ujenzi, linganisha bei zao, na uweke kila oda ya manunuzi kwenye mradi husika.
Mizigo unayoweza kuthibitisha. Bidhaa zinazopokelewa stoo au kufikishwa moja kwa moja kwenye eneo la ujenzi zinarekodiwa dhidi ya oda, hivyo upungufu au ucheleweshaji unaonekana kabla haujasimamisha kazi.
Stoo za ghala na za maeneo ya ujenzi. Ona kiasi cha saruji, nondo na mbao kilichopo kila stoo au kila eneo la ujenzi, kihamishe kati ya maeneo, na urekodi kile ambacho kila mradi umetumia, hadi namba ya utambulisho ya zana na vifaa.


Jua faida yako kwa kila mradi
Toza kulingana na mikataba yako. Toa ankara kwa hatua za mradi, kwa maendeleo ya kazi au dhidi ya malipo ya awali, na utoe risiti zinazokubalika na TRA kupitia muunganisho wetu wa VFD.
Gharama za nguvu kazi zilizo sahihi. Wasimamizi hurekodi saa za timu kwa simu wakiwa eneo la kazi, na saa hizo zinaingia moja kwa moja kwenye gharama za mradi.
Bajeti dhidi ya matumizi halisi, kwa kila mradi. Weka bajeti ya kila mradi na uilinganishe na matumizi halisi ya vifaa, nguvu kazi na wakandarasi wadogo wakati bado kuna muda wa kuchukua hatua.
Usaidizi unaoendelea baada ya kukabidhi.
Kasoro na maombi ya huduma, yanafuatiliwa. Rekodi malalamiko ya wateja na kazi za dhamana kama tiketi, tuma fundi kwa kazi ya huduma ya eneo, na uweke kumbukumbu ya kila ziara kwenye kila jengo.


Zana ambazo timu yako
hutumia kila siku.
Nukuu za bei kwa viwango vyako
Andaa nukuu za bei kwa kila zabuni.
Rekodi za saa za timu
Rekodi saa kwa kila mfanyakazi, kwa kila kazi.
Uwazi wa stoo
Kiasi na mienendo ya mzigo papo hapo kwa kila stoo na eneo la ujenzi.
Ankara zinazokidhi TRA
Ankara za wateja zenye risiti za VFD ndani yake.
Upangaji wa timu na vifaa
Panga nani na nini kinaenda eneo lipi, na lini.
Ufuatiliaji wa zabuni
Fuatilia maulizo na zabuni kuanzia simu ya kwanza hadi mkataba uliosainiwa.